Skip to content

Wala Badali Sioni

Nyuni ya Layali
Ewe nyumi ya layali
pokea zangu salamu
miye kula huwa sili
menivamu muadhamu
kama nanga ya jabali
nimezidiwa ghulamu.

Barua yangu pokea
uyasome yalo humu
yapate kukuelea
yakuingie timamu
mno tena niwilia
kisoma zangu salamu.

Nijile kwako, mwandani,
ni uswahibu napenda
meambatana na ini
mahaba yamenikunda
kama nswi baharini
na kwangu yamenitanda.

Wala badali sioni
kwa huku kutatizana
metuva kote tundani
na pia sikumuona
ila ni wewe changoni
mpenzi meambatana.

Changoni meambatana
waniumiza zumbembe
shamshamu meshikana
yamemea kama pembe
dirika dirika nana
zanifumbe zako ‘kombe.

Bird of the Nights
O you bird of the nights,
receive my greetings.
I do not eat at all.
You have penetrated me, proud one,
like an anchor into a rock.
I, your slave, am conquered.

Accept my letter,
read its contents,
so that it may be clear to you,
and enter your mind entirely,
forgive me many things again,
while reading my greetings.

I came to you, my friend,
it was your friendship I needed,
you embraced me round the waist.
Love has enveloped me
like a fish by the ocean,
and has covered me all over.

Nor do I see any change,
in this getting entangled in one another.
I grazed everywhere in the fruit,
and I have seen no other one
except you; in the belly,
my lover, you embraced me.

In the belly you embraced me,
you hurt me, my lover,
you held me with great strength,
it shone like ivory.
Come, come, my girl,
let your lips enfold me.

—unknown Swahili author, translated by Jan Knappert in the anthology Chagua la Maua, or A Choice of Flowers

Post a Comment

Your email is never published nor shared.